
KDCU WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO LINDI MWAMBAO, KUJIFUNZA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA
Wanaushirika kupitia chama kikuu cha ushirika Karagwe District Cooperative Union (KDCU) wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Ndugu Faxon J. Mbyemeire pamoja na Mrajis Msaidizi mkoa wa Kagera Ndug Edmund Massawe Leo tarehe 12.11.2026 wamefanya Ziara ya Mafunzo katika Chama kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao LTD (LMCU).
Lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kubadilishana uzoefu katika sekta ya ushirika, hususani kujifunza namna chama Kikuu cha ushirika Lindi Mwambao kinavyohudumia wakulima kupitia mfumo wa Stakabadhi za ghala pamoja na uwekezaji uliofanywa katika kuimarisha shughuli za Chama na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wakulima.