UPATIKANAJI WA PEMBEJEO NA HUDUMA ZA UGANI
Chama huratibu upatikanaji wa pembejeo za kilimo (viuatilifu, vifungashio, mizani za kidijitali) na kutoa huduma za ugani kwa Wanachama na wakulima kupitia AMCOS.
Chama huratibu upatikanaji wa pembejeo za kilimo (viuatilifu, vifungashio, mizani za kidijitali) na kutoa huduma za ugani kwa Wanachama na wakulima kupitia AMCOS.
Chama kinasaidia usafirishaji na uhifadhi salama wa mazao ya biashara ya Wanachama — korosho, ufuta na mbaazi — kwenye maghala yake.
Chama huratibu uuzaji wa mazao ya Wanachama kwenye masoko yenye uhakika na kusimamia malipo kwa wakulima kwa wakati baada ya minada.
Kupitia SACCOS ya Wanachama na ushirikiano na mabenki, Chama kinawezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na mikopo yenye masharti nafuu kwa Wanachama na wakulima.
Chama hutoa elimu na mafunzo kwa viongozi na watendaji wa AMCOS pamoja na wakulima ili kuboresha uzalishaji, usimamizi na ujasiriamali.
Chama kinatambua umuhimu wa kuchangia maendeleo ya jamii, ikiwemo kuwezesha huduma za afya kwa wakulima na kutenga sehemu ya mapato kwa shughuli za kijamii katika eneo lake la kazi.